HII NDIO SHERIA ALIYOITUMIA RAIS MAGUFULI KUMSAMEHE BABU SEYA NA MWANAWE PAPII KOCHA
Na:Kione Hamis Mahuruku
Katika sherehe za Uhuru wa Tanganyika za mwaka huu wa 2017
iliyozoeleka kama Tisa Disemba(9 December),Watanzania walio wengi wamepigwa na
Butwaa lakini wengine wakitafakari namna Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe
Magufuli alivyoweza kuwapa Msamaha Wanamuziki Nguza Viking(Babu Seya) na
mwanawe Papii Kocha waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha Jela.
Ameitoa wapi nguvu hiyo Mheshimiwa Rais Magufuli?!
Kumbe Mheshimiwa Rais amepewa nguvu Kikatiba.
KATIBA YA TANZANIA
SURA YA 2 SEHEMU YA 1
Ibara ndogo ya (1),
Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara
hii,Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a)Kutoa msamaha kwa mtu yeyote alliyepatikana na kosa
lolote,na aweza kutoa Msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti,kwa
mujibu wa sharia.
(b)Kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote
aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize adhabu
hiyo wakati wa muda maalu.
(c)Kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yoyote kwa kosa
lolote iwe adhabu tahafifu.
(d)Kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa
mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu
ya kutoza,au kuhozi(au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo
kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Ibara ndogo ya (2),
Bunge laweza kutunga sharia kwa ajili ya utaratibu
utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa ibara
hii.
Ibara ndogo ya (3),
Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa na
kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa Tanzania Zanzibar kwa
mujibu wa sharia iliyotungwa na Bunge na inayotumika Tanzania Zanzibar,hali
kadhalika,maasharti hayo yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa
Tanzania Bara kwa mujibu wa sharia.
No comments: