KOFIA MPE ASLAY KIBA NA DIAMOND WAMEKALISHWA ILA HAJAWAFIKIA
Na Kione
Hamis Mahuruku.
Ni ukweli
usiopingika kwa mwaka 2017 katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva huyu ‘Mtoto’
Aslay Isihaka amefanikiwa 100% kwa kila kitu katika Muziki wake.Ameweza kukonga
Nyoyo za watu wengi mno na kila mtu amemkubali huyu Dogo kutokea katika kizazi
cha Mkubwa Fella.Mbinu ya bandika bandua aliyoitumia huyu dogo katika mtiririko
wa kuachia ‘Mijisongi’ yake si ngeni kwani hata Mtoto wa Tandale Nasib Abdull
huwa anafanya sana.Lakini kitu cha ziada alichofanya Aslay ni namna ya kuimba
nyimbo zinazogusa Mioyo ya watu moja kwa moja.
Alipotoa
wimbo wa Mama alikuwa kama alijua kutokana na hali ya kufiwa na mama yake,aachie
wimbo uliakisi maisha yake kwa kipindi hicho.Heshima kubwa zimuendee Meneja wake
Chambuso na Mtayarishaji ama Watayarishaji wa Muziki wako(Producers) maana
inavyoonekana mnasikilizana sana.Mwenyezi Mungu awasimamie muendelee kutawala
tena mwaka 2018 japo si jambo rahisi.
Kwa nini tumpe
Kofia Aslay? Bwana mdogo ameonyesha katika maisha hakuna linaloshindikana pale
tu unapodhamiria kufanya unachoamini.Katika Ulimwengu wa Diamond Platnumz na
Alli Kiba ambao ni kama Ulimwengu wa Kabumbu Duniani,Ulimewengu wa Messi na
Ronaldo.Si jambo rahisi kupenya,tumeona wengi wamefeli na wamejipapatua tu
lakini wapi?! Darasa alifanikiwa lakini silaha ya Darasa ni utofauti wa style
ya Muziki wake.Kwa Aslay yeye anafanya aina ya Muziki waufanyao Diamond na Kiba
tena mwaka ambao kulitokea vita ya ZILIPENDWA vs SEDUCE ME!
Noma sana
lakini Dogo akatusua na ‘Jisongi’ baab’
kubwa la NATAMBA.Na kweli Aslay katamba sana mwaka 2017.Jipange tena na tena.Tunajua
Silaha yako kubwa ni Tungo mwanana na sauti ya upole na yenye
kuvutia.Usivimbishwe Kichwa na watu wanaokusifia
na kukujaza ujinga kwamba wewe ni Zaidi ya kaka zako Kiba na Diamond.La hasha!
Bado mnooo kuwafikia,ila uwezo unao ongeza hasira utafika mbali Zaidi.
Kwa mwaka huu 2018
nadhani unahitaji sasa kupanua wigo wa Muziki wako,ni wakati wa kujitoa na hata
kulazimisha Collabo za nje.Jitazame mara kadhaa katika Kioo halafu jiulize
swali hili.’Mimi ndiyo yuleyule Dogo Aslay wa Yamoto Band?’ Ukishapata jibu
jiulize swali lingine hili hapa.’Aslay wa mwaka 2017 atapotea au ataimarika
mwaka 2018?’ Kisha maliza na swali hili.’Aslay ndiyo mimi,nilikuwa na mapungufu
gani japo nililishika Soko la Bongo Fleva mwaka 2017?’
Fanyia kazi hayo
maswali kisha simamia Nidhamu yako uliyo nayo,songa mbele.Kitaa Kinaongea,Aslay
amekuwa mkubwa lakini usijifananishe na Kiba na Diamond.Hao ni kaka zako
wamekupita kila kitu,jifunze mazuri kutoka kwao utafanikiwa Zaidi na Zaidi.
By Kione Hamis
Mahuruku.
No comments: