Header Ads

Header Ads

IMANI PAPA CUP KUJA KIVINGINE

Kwa wakazi wa maeneo ya Kibaha mkoa wa Pwani hasa maeneo ya Maili moja,Picha ya Ndege,kwa Mathias na hata maeneo ya Kiluvya ukiongelea mashindano ya mpira wa miguu yaliyotikisa sana kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita bila shaka watakuambia ni mashindano ya ‘IMANI PAPA CUP’.Mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Bwawani Maili moja hakika yalikonga Nyoyo za wapenda Kandanda wote wa ukanda huo wa Kibaha.Sasa wanaambiwa wakae tayari,mashindano hayo yanarudi huku yakiwa yamefanyiwa maboresho makubwa ifikapo mapema mwaka 2018.

         Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kuibua na kuviendeleza vipaji vya Wachezaji soka wa Kibaha na Pwani kwa ujumla.Yalifanyika mwaka 2014 huku yakikosekana  kwa miaka iliyofuatia ukijumuisha na mwaka huu.Akiongea na Heka heka Dimbani, Mratibu wa mashindano hayo Bi.Imani Hamis Papa pichani ambae pia ndiye Bosi wa kampuni ya Imani Papa Entertainment ambao ndio waandaji wa mashindano hayo,alizitaja sababu za kutofanyika kwa mashindano hayo kwa mwaka 2015,mwaka 2016 na mwaka 2017.
         Amesema sababu kubwa ni mbili tu zilizofanya mashindano hayo yasimame kwa kipindi hiki cha miaka mitatu.Mwaka 2015 sababu ilikuwa Uchaguzi mkuu ikafanya mashindano hayo yasifanyike huku sababu ya pili ikiwa ni ukosefu wa Wadhamini wa mashindano kwani amesema walioahidi wengi hawakutekeleza na kupelekea mwaka 2016 na mwaka 2017 yasifanyike pia.’Tumepata Mwarobaini wa kuyarudisha kwa nguvu mashindano haya kwani Watu wa Kibaha wanapenda sana mpira na tayari tumejipanga ili mwakani mapema yafanyike’alisema Bi.Imani Papa.
       Amesema mashindano yajayo wataongeza zawadi na wigo wa Timu shiriki zitaongezeka,kwani msimu wa kwanza Timu zilikuwa za Kibaha tu na zilikuwa na idadi ya Timu kumi na mbili lakini msimu ujao hata Timu za Wilaya nyingine zitaruhusiwa ili kuongeza msisimko zaidi.Msimu wa mwaka 2014 Timu bingwa ilikuwa Timu ya Mwanalugali FC iliyojishindia seti ya Jezi zenye thamani ya Shilingi Laki mbili na Elfu Arobaini huku nafasi ya pili ikitwaliwa na Timu ya Super Eagle iliyopata seti ya Jezi zenye thamani ya Shilingi Liki moja na Elfu Ishirini.
 Bila uchoyo wa fadhilia,Bi.Imani Papa amemshukuru Mbunge wa Kibaha mjini Mh.Syvester Koka na aliyekuwa MNEC wa Kibaha mjini ndugu Rugemalila Rutatina kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa hadi mashindano hayo yamekamilika.Lakini pia ameendelea kuwaomba Wadau wote wanaoweza kusaidia kutoa udhamini watumie namba hii 0717 026 468 au Email hii( imanipapa@gmail.com) ili waweze kupeana utaratibu zaidi.

No comments: