NDANDA KUCHELE NAPITA NJIA-AHMAD MSUMI
Katika maisha ya Soka,mara zote kila Mchezaji amejiwekea malengo yake ili kuhakikisha anazifikia ndoto zake.Kwa Tanzania wachezaji wengi chipukizi,wanajituma sana ili Simba,Yanga na Azam zimuone akafanye maisha.Na mwishowe huenda hata akachome Mahindi benchi na kupotea kwenye Ramani ya Soka lakini yote ni malengo ya mtu aliyejiwekea.Miongoni mwa vijana wanaotafuta maisha kupitia Miguu yake na si kwingine ni katika Soka ni Ahmad Msumi.
Clan TV Online haikusita kuongea na Chipukizi Ahmad Msumi,winga matata anayekipiga katika timu ya Ndanda ya Mtwara.Dogo ama waweza kumwita Yosso anayetumia mguu wa kushoto amesema msimu huu amedhamiria aisaidie sana Timu yake ya Ndanda ili msimu huu iwe miongoni mwa Timu zitakazoshika nafasi ya juu lakini lengo lake pia ni kuhakikisha anafanya vizuri yeye kama mchezaji binafsi ili pate nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya Tanzania.
Msumi aliyejengeka kimichezo anasema,ligi kuu ya VPL kwa sasa yeye si mgeni nayo bali kilichobaki ni yeye kuonyesha kipaji chake.Anasema yuko chini ya Meneja anayejua kuwasaidia na kuwaongoza Wachezaji ili wafikie malengo yao.Amemtaja Meneja wake ni Jamal Kisongo,jamaa anayewasimamia Mbwana Samatta,Thomas Ulimwengu,Rashid Mandawa na Haji Ugando.Anasema kazi imebaki kwake yeye tu kupambana ili awe katika msimu bora.
Msumi anasema maisha yake ya soka alianzia katika timu za mtaani Temeke na baadae akajiunga na Timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na ndipo baadae akajiunga na Ndanda.Anakiri kufuatwa na baadhi ya Viongozi wa Simba msimu uliopita ili ajiunge na Wekundu wa Msimbazi lakini wakashindwana kidogo.
‘Umri wangu bado unaniruhusu kupambana nifike mbali,siwezi kubweteka kwa nini nikate tamaa? Alihoji Msumi kijana aliyezaliwa mwaka 1996Temeke Jijini Dar Es Salaam katika Familia ya Mzee Msumi na Mama Bi.Kulwa.Clan TV Online inamtakia safari njema ya maisha ya soka Ahmad Msumi ili afikie Ndoto na malengo yake.

No comments: