FEDHA MWIBA MCHUNGU KWA YANGA MWAKA 2017
Na Kione
Hamis Mahuruku.
Ukiitazama vizuri Yanga huioni kama ni
Timu hasa iliyojiandaa kwa kugombania Ubingwa au kushindana katika Klabu Bingwa
Afrika.Mtu akikuuliza kwa nini? Jibu lake ni jepesi tu…..! Yanga hawana
Fedha.Ndio,kwa nini Fedha? Yanga kwa mwaka 2017 ni mwaka mchungu kwao hasa kipindi
kile aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji alipokuwa matatizoni na Serikali.Ikapelekea
Yanga ipoteze mwelekeo hasa ikizingatiwa Manji ndio alikuwa kila kitu.
Kukosekana kwa Fedha kwa Klabu ya
Yanga ndio inapelekea leo hii wawe katika kujilaumu,kutupiana lawama na hata kuwachukia
Zaidi watu wenye kariba ya mtazamo wa Mzee wao Akilimali.Pamoja na kukosa Pesa
kwa Yanga,lazima Yanga wenyewe wajipe pongezi ya uvumilivu.Wameweza kuvumilia
hali yote hiyo na hata kufikia kuwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.
Kuna kitu nilikiona kwa Yanga,na
hata siku moja katika vikao vyao na Waandishi wa Habari nilimuuliza Msemaji wa
Timu ndugu Dismas Ten pamoja na Katibu mkuu Mwalimu Boniface Mkwasa juu ya
utaratibu wa usajili wao.Swali langu nilitaka kujua,kwa nini Yanga imemuongeza
Yohana Nkomolwa wakati tayari ina “Watoto” kama Said Mussa,Yusuf
Mhilu,Akilimali na hata Mwashiuya japo ana uzoefu na ligi? Lengo lenu ni nini
Yanga wakati mnakabiliwa na mashindano magumu ya Klabu bingwa Afrika,ikiwa
mnajua wachezaji wenu Ngoma,Tambwe,Kamusoko ni majeruhi?
Na je,kulikuwa na ulazima gani wa
kuongeza vijana katika kikosi wakati tayari vijana mnao na hamjaanza kuwatumia
ipasavyo? Kwa nini nafasi hiyo msitumie kuongeza walau “Striker” mmoja
aliyekamilika”matured”? Lakini nikaonekana kama simpendi Yohana Nkomolwa na
Yosso wengine wa Jangwani.Mimi ni muumini mkubwa wa watoto wadogo lakini lazima
tukubali,kwa sasa Yanga haikuwa na hitaji la kuongeza watoto kikosini.Yanga
ilihitaji Zaidi wachezaji waliokamilika ili wawapambanie kikamilifu katika
mashindano yanayowakabili.
Kwa mwelevu utabaini na kung’amua
kwamba inshu haikuwa mipango ya kuongeza wigo kwa vijana ndani ya Klabu,bali
shida ilikuwa Fedha.Fedha imepelekea kuwakosa Wachezaji wengi wa kiwango cha
juu wenye hadhi ya kuchezea Yanga na si Wachezaji wa kuja kujaribiwa Yanga.
Jana baada ya kufungwa na Mbao
magoli mawili kwa sifuri magoli ya ‘Kinda’ Habib Kyondo nadhani Yanga watakuwa
wamegundua kwamba ni aina gani ya Washambuliaji walio nao.Tegemezi lilikuwa kwa
Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib nao hawakuwepo kikosini kwa sababu tofauti.
Iwapo Yanga wangekuwa na
Washambuliaji wengine wa kariba ya Ajib na Chirwa wangeendelea kuwa Wateja wa
Mbao katika Dimba la CCM Kirumba? Kabla hujatazama mbinu na uwezo wa Mwalimu
msaidizi wa Yanga Shedrak Nsajigwa kwanza angalia uwezo wa Wachezaji wa Yanga
waliocheza jana.
Yanga ni wavumilivu,endeleeni
kuwaombea Wachezaji walio na majeraha warejee mapema maana Klabu Bingwa Afrika
ni hatari Zaidi kuliko hayo mashindano ya Mapinduzi.
No comments: