HUMJUI MISS KK….? HUYU HAPA!! ANAZINDUA NGOMA YAKE’WANANUNA’!!
Na: Kione Hamis Mahuruku.
Ukimtazama
utapenda kumuangalia muda wote jinsi alivyo mcheshi,na zaidi hatokuboa
kabisa,na ni Msela haswa kimuonekano.Ni Rapa mkali mwenye kujua nini
anachokifanya,na anajua thamani ya Muziki aufanyao.Ni Latifa Mussa au kwa jina
lake la kutafutia Mkate anajulikana zaidi kwa jina la Miss KK.Kwa wanaofuatilia
Muziki wa Bongo Fleva kwa sasa si jina geni Machoni na Masikioni mwao.
Miss
KK ana ujio mpya sasa,siku ya Jumamosi Tarehe 24/2/2018 atazindua Wimbo wake
mpya kabisa.Wimbo unaoitwa ‘Wananuna’,atazindua Audio na Video.Uzinduzi huo
utafanyika katika Hoteli ya Pallet maeneo ya Mbezi Beach.’Nimeona na mimi
nifuate Nyayo za Watanzania wenzangu kuzindua
Audio na Video kwa pamoja,kule South Afrika huwa tunaanza kuachia Audio
na baadae Video.Imebidi nikae na kuusoma Mchezo wa hapa Home pia’.Alisema Miss
KK.
Amesema kwa sasa amebadili Menejimenti na
atakuwa chini ya Kampuni ya KOI Entertainment na Meneja wake ni DJ Kinywele
pamoja na usimamizi wa karibu kabisa kutoka kwa Kampuni ya WANENE ENT.Amesema
pia,Show hiyo ya uzinduzi itaanza saa moja za jioni hadi usiku
mkubwa.Watakaofika mapema saa moja hadi saa tatu usiku watapata Complimentary
kwa na Vinywaji.Lakini watakaochelewa watachangia kiingilio cha Elfu
Tano(5,000/-) kwa mtu mmoja.
Miss KK anasema zaidi kwamba, ameshapata
uzoefu mkubwa katika Muziki kwa sasa.Mwaka 2015 nilianza kwa kuachia Ngoma
yangu iliyoitwa ‘Anginandaba’ ambao kwa Kiswahili unamaanisha ‘Sijali’ au kwa
Kingereza ‘I don’t care’.Ngoma hiyo iliingia katika chati za Radio ya Gagasi FM ya Durban na nikaitwa kwa
mara ya kwanza katika Interview na kupata idadi kubwa ya Mashabiki.Alisema Miss
KK.
Baadae nikaachia Ngoma
mfululizo ambazo ni Getting lit,Baridi tu na Kata Kiuno.Baadae Ngoma kufanya
vizuri kule South Afrika,ndipo nikapata ushauri na Watu mbalimbali nikashauriwa
nigeukie nyumbani Tanzania.Ndipo mwezi Disemba mwaka 2016 ikanilazimu nirudi
Bongo na kuanza Mchakamcha wa kujitambulisha hapa nyumbani.Alhadullillah kwa
sasa nimeanza kufahamika sana lakini hapo mwanzoni ilikuwa ngumu sana watu
kunielea.Alieleza Miss KK.
Kubwa Zaidi alisisitiza kwamba
kutakuwa na Wasanii wengi watakaomsindikiza katika uzinduzi huo pamoja na
Wasanii wanaomilikiwa na Kampuni ya WANENE ENT.Amesema kwa mtu atakayekwenda
PALLET HOTEL,ukitokea Kawe unapita ilipo Radio TIMES FM mbele kidogo ukiuliza
utafika.Ameomba Watu wajitokeze kwa wingi wakakate kiu ya Burudani.Kwa taarifa
Zaidi pia fuatilia Clan TV Online.
No comments: